February 28, 2013




Wakati mjadala wa chenga kali aliyompiga nahodha wa Barcelona, Cares Puyol kabla ya kusababisha bao la pili wakati Real Madrid ikiishinda kwa mabao 3-1, sasa Angel Di Maria ataikosa mechi nyingine ya El Classico.

Zinapokutana Real Madrid na Barcelona ndiyo El Classico, mechi ijayo ni kesho Jumamosi na Di Maria hatacheza kutokana na kulambwa kadi nyekundu baada ya njano mbili katika mechi ya mwisho ya La Liga, pale timu yake ilipoivaa Deportivo la Coruna.

Madrid imefanya kazi ya kukataa rufaa ili Di Maria acheze mechi hiyo, lakini imegonga mwamba na kadi mbili njano za mwamuzi Álvarez Izquierdo, moja ikiwa ni ya kuutupa mpira kwa hasira ya pili kukaa mbele ya ukuta pamoja na kuelekezwa na mwamuzi, zimeonekana ni sahihi.

Huenda Jose Mourinho akaamua kuanza na Mbrazil, Kaka katika nafasi hiyo ili kuendelea kuipa presha Barcelona ambayo itakuwa imepania kulipa kisasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic