February 28, 2013




Pamoja na kuendelea kuwa tishio msimu huu na uliopita, imeelezwa kiungo nyota wa Tottenham Hotspur, Garreth Bale amekuwa akivaa soksi maalum uwanjani.

Soksi anazovaa Bale zinajulikana kwa jina la Trusox na zinatengenezwa nchini Marekani, kwa kiasi kikubwa ndizo zinamuongezea kazi.


Soksi hizo zinaelezwa kumsaidia mchezaji kutopoteza nguvu hata kidogo, badala ya kuongeza mwendo.

Kitu Kingine, soksi hizo ambazo bei yake ni pauni 25 (Sh 63,750) ni bora kwa kulinda kifundo cha mguu maarufu kama enka.

Kwa wachezaji wenye kasi kama Bale, soksi hizo zimekuwa ni msaada mkubwa kwani kasi ya wachezaji kuzitumia imekuwa ikiongezeka.

Wengine ambao wanatumia soksi hizo ni pamoja na Demba Ba na Victor Moses raia wa Senegal na Nigeria wanaokipiga katika klabu ya Chelsea ya London.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic