February 27, 2013




Tokea ameachwa Man United, mshambuliaji Dimitar Berbatov wa Fulham amekuwa akionyesha uwezo mkubwa wa kupachika mabao.

Raia huyo wa Bulgaria, pamoja na uwezo soka, hivi karibuni amewashangaza watu wengi baada ya kuonyesha ana uwezo mkubwa sana uchoraji.

Hakuna ubishi picha alizochora kutumia kalamu ya mkaa, Berbatov ameonyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwachora watu wengi nyota duniani.

Pamoja na kuwachora watu wanaohusika na mambo mbalimbali, lakini ameonyesha ni shabiki wa miondoko ya hip hop baada ya kuwachora wakali wawili wa miondoko hiyo marehemu 2Pac Shakur na Snoopy Dogg Doggy.


Pia amethibitisha yeye ni shabiki wa filamu za kibabe, baada ya kumchora Bruce Wills, mmoja wa waigizaji wa Hollywood anayesifika kwa kuigiza filamu za aina hiyo.

 Berbatov aliziweka picha hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook huku kukiwa na picha yake inayoonyesha akiwa na kalamu hiyo ya mkaa sikioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic