February 27, 2013




Viungo Athuman Iddi ‘Chuji’na Haruna Niyonzima wataanza kazi  ya kupiga mipira ya faulo katika mechi kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Kocha Mkuu, Ernie Brandts amesema tayari walianza mazoezi kwa siku kadhaa na wachezaji wanne watakuwa wakifanya kazi hiyo.

Pamoja na Chuji na Niyonzima wengine ni mabeki Mbuyu Twite na Oscar Joshua.
Chuji na Niyonzima watapiga faulo zote zinazotakiwa kupigwa kwa mguu wa kulia, huku Oscar na Mbuyu watafanya kazi hiyo watakapopata faulo za mguu wa kulia.

“Katika mechi ya leo, iwapo faulo zitatokea, jukumu litakuwa ni lao na watakachofanya ni kujadiliana na mwisho ni kutumia uwezo wao na mafunzo waliyipata,” alisema Brandts.

Mechi ya leo ni muhimu sana kwa Yanga ambayo inahitaji ushindi ili kufikisha pointi 42 wakati Kagera yenye pointi 27 katika nafasi ya tano, inataka kupanda juu kwa kupata pointi tatu muhimu.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Oktoba 8, 2012 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Themi Felix katika dakika ya 68.

Maana yake,  Yanga leo itakuwa inapambana kupata pointi hizo muhimu lakini kulipa kisasi pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic