February 27, 2013




 EXCLUSIVE PICTURE...
Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic ameondoka katika ardhi ya Tanzania baada ya kukwea pipa leo saa 10:30 alfajiri.
Milovan aliyewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), alizungumza na mtandao huu na kueleza mambo mengi kuhusiana na Simba.

Kila kitu alichoeleza Milovan kuhusiana na maisha yake wakati akiwa Simba kitawekwa hewani.

Kocha huyo ambaye amelipwa fedha zake dola 32,000 na nyongeza ya dola 3,000 kutoka kwa Malkia wa nyuki ameanika mambo mengi sana.
Lakini amerudia tena kuwashukuru mashabiki wa Simba kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa na anawatambua kama ndugu.

Kocha huyo ameondoka na rekodi ya ubingwa Simba ikiwa ni pamoja na rekodi kubwa ya ushindi ‘mnene’ wa mabao 5-0 dhidi ya watani wao Yanga, msimu uliopita.

Milovan aliondoka na dege la Shirika la Ndege la Uturuki na anatajia kutua Belgrade, Serbia leo na ataunganisha safari ya takribani saa mbili kwenda katika mji aliozaliwa wa Cacak unaotamkwa chachak.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic