February 26, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ameamua kufanya kazi ya kuwanoa wachezaji wanne ambao watakabidhiwa kupiga mipira ya faulo maarufu kama ‘iliyokufa’.

Brandts raia wa Uholanzi amesema tayari ameanza kazi hiyo kwa kuwa anataka kikosi chake kiendelee kukamilika kila idara kila siku zinavyosonga.
“Kawaida katika timu unaimarisha mambo hatua kwa hatua, hivyo sasa tumefikia wakati wa kutengeneza wapiga faulo wa uhakika.

“Nitateua wachezaji wanne ambao nitakuwa nikifanya nao kazi hiyo kila ninapokuwa na nafasi ili kuhakikisha ikitokea faulo, tunaangalia iko upande gani na anapiga nani,” alisema Brandts.

Kabla ya hapo, Athumani Idd ‘Chuji’ na Oscar Joshua ndiyo waliokuwa wakipiga faulo nyingi za kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic