Pamoja na kulipwa fedha zake, kocha
wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic amesema anaondoka nchini akiwa na majonzi
makubwa.
Milovan raia wa Serbia amesema
kulipwa fedha zake kwa maana ya maslahi lilikuwa ni jambo muhimu sana, lakini
urafiki wake na watu wa Simba ni muhimu zaidi moyoni mwake.
“Naona naondoka nawaacha rafiki
zangu wa kweli, angalia mashabiki walivyoniunga mkono kuanzia mwanzo hadi. Tokea
nikiwa na timu hadi wakati wa matatizo.
“Mashabiki wa Simba walikuwa na
ujasiri mkubwa, ingawa kuna baadhi ya viongozi walionyesha chuki ya wazi dhidi
ya yangu, lakini bado wao waliendelea kuonyesha upendo.
“Nasikia faraja kwa kuwa zaidi ya
watu milioni waliniunga mkono na wawili au watatu tu wakaonyesha chuki kwangu,
haliwezi kuwa suala gumu kwangu. Nitaendelea na mambo yangu na sitaacha
kuikumbuka Simba kwa kuwa wengi wao wananipenda.
“Naipenda sana Simba, wakati
mwingine natamani ingekuwa kwetu Serbia. Lakini maisha ndivyo yalivyo, siku ya
mwisho mambo hubadilika na unatakiwa kukubali.
"Wako ambao sasa wananishambulia, najua hawakupenda nipate haki yangu, lakini inawauma ninavyosema ukweli. Siku wakitulia watakubali ninachokisema kwa kuwa wanakijua na wanaelewa kilivyotokea, mimi si mgomvi, pia sipendi malumbano” alisema Milovan.
Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharusi
alijitolea kumlipa MIlovan fedha dola 32,000 alizokuwa anaudai uongozi wa Simba
ambao ulikuwa ukimzungusha huku viongozi wake wakiendelea kutoa ahadi.
Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuki
alitoa kitita cha dola 35,000 ikiwa ni dola 3000 zaidi ya alichokuwa anadai
kocha huyo na tayari ameishapokea fedha zake.
0 COMMENTS:
Post a Comment