February 28, 2013



 Saleh Ally, Brandts na Shigongo..

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts muda mfupi uliopita alifanya ziara fupi katika ofisi za gazeti maarufu la michezo nchini Tanzania, Championi.

Brandts raia wa Holland, alifika katika ofisi za Championi leo asubuhi na kuzungumza na Mhariri Kiongozi, Saleh Ally ambaye baadaye alimtambulisha kwa wahariri wa gazeti hilo, John Joseph (Championi Ijumaa), Phillip Nkini (Championi Jumatano) na Ezekiel Kitula anayekaimu Championi Jumatatu.

Akiwa na Shigongo...

Akiwa na Mariri wa Championi Ijumaa, John Joseph 'JJ'..
 
Baada ya hapo, Brandts alikaribishwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo ambaye pia ni mwanamichezo.

Shigongo ambaye ni shabiki mkubwa wa soka, kikapu na ngumi alibadilisha mawazo na Brandts kwa takribani nusu saa na baada ya hapo akatambulishwa kwa waandishi wa Championi ambao ni marafiki zake pamoja na Meneja Mkuu wa GPL, Abdallah Mrisho maarufu kama Abby Cool.
Meneja wa GPL, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) akiwa na Brandts pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa Championi...

Ziara ya Brandts katika gazeti hilo ni kutokana na kukubali namna ambavyo limekuwa likiripoti kuhusiana na maendeleo ya Yanga pamoja na nyingine za soka na michezo mingine bila ya upendeleo.
Brandts alisema anavutiwa na Championi kwa kuwa vitu vingi wanavyoripoti wanavifuatilia kwa karibu, mara nyingi waandishi wake wanajitokeza mazoezini na mengi wanayajua kwa kufuatilia kwa karibu.

Kuhusiana na kukosoa, Brandts alisema hana hofu na hilo hasa kwa kuwa mara nyingi ukosoaji wa gazeti hilo unaendana na hali halisi.

Hii ni mara ya pili makocha kutembelea Championi ndani ya siku saba, wiki iliyopita aliyekuwa Kocha Mkuu, Milovan Cirkovik alitembelea ofisi hizo na kuangalia uaandaaji wa gazeti unavyokwenda.
Kabla ya hapo, Kocha Mkuu wa Harambee Stars, Adel Amrouche raia wa Ubeligiji mwenye asili ya Algeria naye alitembelea ofisi za gazeti hilo wakati kazi ya uandaaji wa Championi Jumatano ikiendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic