BRANDTS AKIWA NA MMILIKI WA SALEHJEMBE, SALEH ALLY ALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM, JANA.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesisitiza bado
timu yake inasumbuliwa na ugonjwa wa wachezaji wake hasa washambuliaji
kutozitumia nafasi za kufunga wanazozipata.
Brandts
raia wa Uholanzi amesema huo ndiyo ugonjwa mkubwa katika kikosi chake na
amekuwa akiendelea kuufanyia kazi kwa juhudi kubwa.
Kocha huyo
ambaye amekigeuza kikosi cha Yanga, ameiambia Salehjembe kuwa iwapo
washambuliaji wake wangekuwa wakitumia vizuri nafasi wanazopata, kikosi chake
kisingekuwa na hofu na mechi yoyote.
“Tuna
kikosi kizuri na wachezaji wangu wanajitahidi sana, ingawa bado tunafanya
mazoezi katika viwanja vyenye viwango vya chini lakini wanaonyesha tofauti
kubwa katika mechi zetu.
“Tatizo
kubwa ambalo naona ni kama ugonjwa ambao nautafutia tiba ni kupoteza nafasi,
hali hiyo hainivutii, lakini bado naendelea kuifanyia kazi.
“Katika
soka mambo mengine yanabadilika baada ya kuyazungumzia au kufanya mazoezi kwa
siku kadhaa na si mara moja au mbili. Hata hivyo, nimekuwa nikisisitiza kwa
washambuliaji kutofanya mzaha na nafasi tunazopata.
“Bado
nina imani nao kubwa, ninaamini watafanya vizuri baadaye. Lakini sasa acha
tuendelee kufanya kazi kwa ajili ya kuleta mabadiliko zaidi,” alisema Brandts.
Kocha
huyo amegeuza uchezaji wa Yanga kwa kiasi kikubwa na hasa uchezaji wa kasi na
pasi za uhakika, hali inayofanya kila kikosi kinachokutana na Yanga kuwa katika
wakati mgumu.
0 COMMENTS:
Post a Comment