March 5, 2013




Vipigo viwili kutoka kwa Real Madrid na kimoja kutoka kwa AC Milan kumeifanya Barcelona iondolewe katika nafasi ya kwanza ya klabu zinazoongoza kwa ubora duniani.

Shirikisho la Kimataifa la Takwimu na Historia (IFFHS), limeishusha Barcelona kutoka kileleni hadi katika nafasi ya tano.
Pamoja na kuendelea kutofanya vizuri, IFFHS wamewapa  Chelsea ya England nafasi ya kwanza, wakifuatiwa na Atletico Madrid ya Hispania.

Wajerumani wa Bayern Munich ambao wananekana kuwa sawa msimu huu wako katika nafasi ya tatu, wakati Corinthians ya Brazil ambao ni mabingwa wa dunia upande wa klabu wako katika nafasi ya nne.

Barcelona imekuwa klabu bora katika chati za IFFHS kwa zaidi ya miaka miwili, hadi wiki tatu zilizopita baada ya mambo kuanza kuwaendea kombe na kujikuta wakikutana na vipigo mfululizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic