March 5, 2013





Baada ya ushindi mara mbili dhidi ya Barcelona, wachezaji wa Real Madrid wameonyesha kuwa na ari na kuamini wana nafasi kubwa ya kushinda katika mechi ya leo.

Madrid tayari wako England kuivaa Man United katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya raundi ya 16 Bora. Mechi ya kwanza mjini Madrid ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kiungo wa Madrid, Mesuti Ozil amesema katika mahojiano vyombo vya habari vya Uingereza kwamba, iwapo walifanikiwa kushinda katika uwanja wa Camp Nou, hawana hofu ya kufanya hivyo wakiwa Old Trafford.

“Kilichotokea Camp Nou si kitu kidogo, tulishinda kwa mabao matatu, utaona ugumu wa pale na tulicheza na timu bora. Kama tuliweza pale hata Old Trafford hatushindwi.

“Kama hiyo haitoshi, ukiangalia mechi yetu ya kwanza dhidi ya Manchester, tulionyesha sisi ni bora zaidi yao. Lakini tumeonyesha hivyo katika mechi mbili dhidi ya Barcelona.

“Bado tunaiheshimu Man United kama timu bora kabisa, lakini utakuwa ni mchezo mgumu sana,” alisema Ozil.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic