Unapokwenda
katika mazoezi ya timu za soka kuna raha yake, pamoja na soka lakini wachezaji
hawaishi vituko ambavyo ni burudani inayojitegemea tofauti na uwezo wanaouonyesha uwanjani.
Pamoja na
kucheza mazoezi yao kwa juhudi au kuwavutia mashabiki wanaojitokeza kutokana na
ushindani, lakini wamekuwa na maneno mengi utafikiri wanaigiza michezo ya kuchekesha.
Mfano,
katika mazoezi ya Yanga wiki, moja ya vituko vilivyojitokeza ni kiungo nyota wa
timu hiyo, Athumani Iddi ‘Chuji’ kushauriwa pamoja na kutokuwa na nywele
katikati ya kichwa chake, eti anyoe kiduku.
Kiduku ni
staili ya kuachia nywele katikati ya kichwa kama ambavyo hufanya mshambuliaji
wa AC Milan, Mario Balotelli.
Wachezaji
wawili wa Yanga, beki Mbuyu Twite na winga, Simon Msuva wana kiduku.
Hivyo
wachezaji wenzake waliendelea kumtania Chuji wakimshauri anyoe kiduku, pamoja
na kwamba anajulikana kwa ubabe, Chuji aliendelea kucheka akionyesha kudharau
alichokuwa anaambiwa.
Kawaida
amekuwa akinyoa nywele zake kuficha ‘walaza’ wake, lakini hivi karibuni, Chuji
ameamua kuachia nywele hizo na sasa unaonekana vizuri kabisa huku akisisitiza
kwamba yeye sasa ni mkongwe, hivyo haitaji kunyoa ‘unga’, yaani kipara kila wakati.
0 COMMENTS:
Post a Comment