Aliyekuwa
Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic aliapa wakati anaondoka na kusema maneno
ambayo huenda sasa yanaanza kuonekana taratibu.
Milovan
raia wa Serbia ambaye alitupiwa zigo kubwa la lawama na viongozi wa Simba,
kwamba ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa Simba, alitoa maneno ambayo dalili zake
zinaanza kuonekana sasa.
Milovan
alisema anachojua viongozi wamekuwa tatizo kubwa sana wakati akiwa mwalimu na
alivumilia mambo mengi sana.
Alisema alivumilia
mambo mengi ikiwa ni pamoja na kunyamaza hata alipolazimishwa kuwachezesha
wachezaji fulani.
Akasema
viongozi wengi wa Simba, wamekuwa na tabia ya kuamini wanajua sana soka bila
hata ya kulisomea, yeye amekwenda shule miaka 11 kusomea mchezo huo. Lakini bado
walitaka kumfundisha nani acheze na nani abaki benchi.
Siku alipokuwa
anaondoka, aliwaachia ujumbe mara mbili. Kwanza akasema hivi: “Kuwa na fedha si
kujua soka.”
Halafu
ujumbe wa pili akasema hivi: “Sipendi malumbano, ila nakuhakikishia muda ndiyo
utakaosema kama kweli mimi ndiyo nilikuwa tatizo au wao, tusubiri.”
Sasa
tayari Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope amejiuzulu na ndiye
alikuwa jembe la usajili la Simba msimu huu.
Pia Makamu
Mwenyekiti, Geofrey Nyanga ‘Kaburu’ ambaye pamoja na lawama nyingi pia alikuwa
na msaada wake mkubwa Simba, ameachia ngazi jana, saa chache baada ya Hans Pope
kuwa amebwaga manyaga.
Hapo ndipo
pa kujiuliza, aliyoyasema Milovan ambaye alirejea Dar na kuanza kusumbukia
malipo yake, ndiyo yameanza kutimia?
0 COMMENTS:
Post a Comment