MALKIA wa
Nyuki ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Simba ambayo
itahakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mechi zilizobaki.
Malkia wa Nyuki ambaye jina lake halisi ni Rahma Al Kharusi, amekuwa msaada mkubwa kwa Simba katika siku za hivi karibuni ingawa inaonekana anaangushwa kutokana na kutokuwa na utulivu na uongozi kuyumba ndani ya klabu hiyo.
Kamati
hiyo iliyoteuliwa juzi kwenye hoteli ya Serana jijini Dar es Salaam tayari
imeanza kumomonyoka baada ya aliyekuwa ameteuliwa kuwa makamu wa kamati,
Geofrey Nyange Kaburu kutangaza kujiuzulu nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa
Simba, sambamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope, jana.
Akizungumza
kuhusiana na kamti hiyo, Malkia wa Nyuki alisema lengo lao nmi kurudisha
ushirikiano na kuisaidia Simba kucheza vizuri na kushinda mechi zilizobaki za
ligi.
“Utaona
kama watu wamekata tama, lakini sisi bado tunaamini kuna kila sababu ya
kuangalia uwezekano wa kufanya vizuri katika mechi zilizobaki.
“Simba
inaweza isiwe na nafasi, lakini ni timu yenye heshima zake. Inahitaji ushindi
kwa ajili ya kuendelea kuonyesha ni timu kubwa.
“Lakini
kingine ni kuepuka kuwaumiza wanachama na mashabiki wanaoiunga mkono. Kuna mengi
ya kufanya, huenda vingine tukavifanya msimu ujao lakini suala la kushinda
mechi zilizobaki ni muhimu sana,” alisema.
Wengine walioteuliwa
katika kamati hiyo ni Katibu Joseph Itang’are ‘Kinesi’, wakati
wajumbe ni Zacharia Hans Poppe, Swedi Nkwabi na Musley Al Rawah.
0 COMMENTS:
Post a Comment