Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa)
limetuma mapendekezo 10 ya marekebisho ya katiba yake kwa wanachama wake kwa
njia ya waraka.
Mapendekezo hayo yametumwa kwa kila
nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320, ambapo wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho
yao ya mabara watapiga kura ya ndiyo au hapa. Kwa upande wa Afrika, wanachama
wa Fifa wanatakiwa kuwasilisha kura zao kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (Caf).
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
amesema leo kuwa baadhi ya mapendekezo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji
kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Fifa (Fifa Congress). Makamu wa Rais wa Fifa
na wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi
wathibitishwe na Fifa Congress.
Muundo wa Kamati ya Utendaji; nafasi
moja ya vyama vya mpira wa miguu vya Uingereza (British FAs) sasa inahamishiwa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa). Pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi
ya FIFA anatakiwa kushiriki vikao vya Kamati ya Utendaji bila kuwa na haki ya
kupiga kura.
Uchaguzi wa Rais; mgombea anatakiwa
kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama wanachama kutoka katika mabara
mawili tofauti. Ukomo wa uongozi; kuanzisha vipindi vya uongozi. Ukomo wa umri;
ukomo wa umri usiozidi miaka 72 wakati wa kugombea utekelezwe.
Uwakilishi wa kutosha kwa makundi yenye
maslahi katika Fifa; makundi yenye maslahi katika mpira wa miguu kama wachezaji
wapate uwakilishi katika Kamati ya Mpira wa Miguu. Uteuzi wa mwenyeji wa
Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi sasa ufanywe na Mkutano Mkuu wa TFF.
Hivi serikali iliitengua katiba mpya ya
TFF iliyopitishwa na wanachama wake kwa njia ya waraka na kutaka iendelee
kutumika ya mwaka 2006.
0 COMMENTS:
Post a Comment