Mshambuliaji
wa AC Milan, Kevin-Prince Boateng na Rais wa Fifa, Sepp Blatter watakutana
mwezi huu mwishoni kujadili kuhusiana na suala la ubaguzi wa rangi.
Fifa
imetoa taarifa ya kuwepo kikao kati ya Boateng raia wa Ghana pamoja na Boateng na
tayari kimepangwa kufanyika Machi 22 jijini Zurich, Uswiss.
Boateng amekuwa
mpiganaji mkubwa wa masuala ya ubaguzi, Januari mwaka huu aliwaongoza wachezaji
wenzake wa AC Milan wakiwa uwanjani kulaani kuhusiana na vitendo hivyo vya
ubaguzi wa rangi.
Boateng amealikwa
katika moja ya vikao vya Umoja wa Taifa (UN) kuhusiana na kupinga masuala ya
ubaguzi wa rangi.
Tayari
Blatter ameshazungumza kwenye vyombo vya habari na kumsifia Boateng kutokana na
alichokionyesha kuhusiana na suala hilo ambalo limekuwa likichukua kasi kubwa hasa
barani Ulaya.
Ubaguzi wa rangi umekuwa tatizo kubwa kuanzia
uwanjani hadi kwa mashabiki ambao wamekuwa wakiwazomea wachezaji weusi kwa
kutumia ndizi au mifano ya masokwe.
Mbaya zaidi, umefikia wakati hadi waamuzi wamekuwa
wakilaumiwa kuhusiana na suala hilo hali inayowafanya wachezaji weusi kuwa
katika hali ya wasiwasi.
Hata hivyo, Fifa ambayo inahusika na soka duniani
kote, imekuwa ikifanya juhudi za dhati kupambana na suala hilo ambalo
linaonekana kuwa na nguvu kubwa katika nchi za Ulaya Mashariki ambao pamoja na
kuwa ndiyo masikini zaidi barani humo, lakini wamekuwa wajeuri na wanaongoza
kwa tabia hizo chafu na za kipuuzi za ubaguzi wa rangi.
0 COMMENTS:
Post a Comment