Watazamaji 13,398 wameshuhudia pambano
la Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Kagera Sugar lililochezwa juzi (Februari 27
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 77,117,000.
Mechi hiyo namba 130 iliyochezeshwa na
Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL
wakiwa na pointi 42 kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 45 na
Haruna Niyonzima.
Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
18,291,297.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
11,763,610.17.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho
kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 11,908 na
kuingiza sh. 59,540,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio
cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 80 na kuingiza sh. 1,600,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 9,300,659.97, tiketi sh. 3,348,990, gharama za mechi
sh. 5,580,395.98, Kamati ya Ligi sh. 5,580,395.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 2,790,197.99 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 2,170,153.99.
0 COMMENTS:
Post a Comment