March 6, 2013


Licha ya kupewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi na kusonga mbele kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza ulipigwa Santiago Bernabou, Machester United jana ilishindwa kuonyesha cheche zake na kujikuta ikikubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Real Madrid na kusukumwa nje ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.

 Dakika ya 48 ya Mchezo huo Mashabiki zaidi ya 80,000 walifurika kwenye Uwanja wa Old Traffod walishudia Sergio Ramos akijifunga Mwenyewe baada ya kushindwa kuudhibiti mpira wa kros uliokuwa umepigwa kutoka wingi ya kushoto na nyota wa Ureno Louis Nani hivyo kuipa Man United Bao la Kuongoza. Hata hivyo Madrid licha ya kufungwa bao hilo haikuonekana kutetereka na mnamo dakika ya 69 Luka Modric aliyekuwa kwenye kiwango bora na kuisumbua sana United sehemu ya kiungo aliisawazishia timu yake baada ya kuachia kombora kali lilokwenda moja kwa moja wavuni.

Dakika Moja baadae nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo alifanikiwa kupachika kimiani bao la pili kwa timu yake baada ya kuwahi kros iliyopigwa kutoka wingi ya kulia na Gonzalo Higuain na kuizima kabisa United ambayo licha ya kufanya mabadiliko kadhaa haikuweza kupata bao la kusawazisha. Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa na mwamuzi wa mchezo huo Real ikaibuka na ushindi wa bao 2-1.

Mara baada ya mchezo huo Kocha wa Real Madrid 'Mbwatukaji' Jose Mourinho aliimbia runinga ya sky kuwa hawezi kabisa kuipima furaha aliyonayo baada ya vijana wake kuibuka na ushindi, ila kilicho kwenye kichwa chake hivi sasa ni nini atafanya kwenye mchezo unaofuata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic