Kama
utani lakini dalili za jela zinanukia kwa mshambuliaji wa Manchester City,
Carlos Teves ambaye amekamatwa akiendesha gari licha ya kuwa amezuiwa kuendesha
kwa miezi sita.
Tevez raia
wa Argentina alikamatwa karibu na kwake eneo la Alderley Edge, Cheshire
akiendesha gari lake bila ya kujali Januari 6, mwaka alifungiwa kuendesha gari
kwa miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya barabarani.
Msemani
wa Polisi wa Cheshire, Tevez mwenye miaka 29 alikuwa amezuiwa kuendesha gari
kwa muda huo lakini amekamatwa tena na sheria inaonyesha adhabu yake ni miezi
sita jela na fedha ya faini pauni 5,000.
Hata
hivyo, Polisi baada ya kumshikilia kwa muda mchache, walilazimika kumuachia
Tevez aendelee na mishe zake baada ya kutokuwa na mtu anayeweza kutafsiri kwa
kuwa hawezi kuzungumza Kingereza.
Tevez
anayejulikana kwa utukutu, ametakiwa kurejea Polisi Jumanne ijayo na ndiyo
itajulikana kama atapelekwa mahakamani au anaweza kuepuka kifungo hicho hicho.
Mara
baada ya Tevez kuzuiwa kuendesha gari, mara nyingi alionekana mitaani au hata
mazoezini akiendeshwa na mkewe. Lakini baada akachoka na hali hiyo na kuamua
kusukuma mwenye ‘mchuma’ wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment