March 9, 2013



Malkia wa Nyuki akiwa na Alhaji Rage..
Tawi maarufu zaidi la klabu ya Simba la Mpira Pesa, limerejea kundini na kutoa ahadi ua ushirikiano mkubwa.
Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharusi ndiye amefanya kazi hiyo ya ziada ya kuzungumza na viongozi wa tawi hilo jana jioni katika kikao kilichomalizika usiku.

Mama huyo ‘mwanajeshi’, maarufu kama Malkia wa Nyuki aliamua kuwarudisha wanachama hao waliokuwa katika mgogoro mkubwa na Mwenyekiti, Ismail Aden Rage aliyetangaza kulifuta.

Lakini baada ya mazungumzo hayo, Mpira Pesa wanaojulikana kwa kuishangilia na kuipa nguvu Simba walisema mambo yatakwenda vizuri na watarudi kushirikiana na uongozi wa Simba kama ilivyokuwa awali ili kuisaidia katika mechi zilizobaki.

Malkia wa Nyuki alifanya kikao hicho na kuwashawishi kurudisha ushirikiano ili kuunda nguvu kubwa kwa Simba ambayo imegawanyika na kufanya iyumbe.

“Nashukuru sana, kikao kimekwenda vizuri lakini watu wa Mpira Pesa wameonyesha ni waelewa na wenye mapenzi makubwa na klabu yao. Wanaumizwa na matokeo mabaya.
“Nimewaomba wakubali tushirikiane kuisaidia Simba katika wakati huu mgumu, 
hawana tatizo na hilo na ndilo jambo la msingi.

“Mambo hayawezi kubadilika na kuwa mazuri kama tukiwa katika makundi, najua muda unatakiwa lakini tukianza kwa kurudisha umoja, basi mambo yatakwenda vizuri tu,” alisema Malkia wa Nyuki.

Malkia wa Nyuki ndiye amekuwa jembe la kuiunganisha Simba ambayo imeyumba huku viongozi wake wakianza kujiuzulu mfululizo ingawa Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage amekuwa mgumu kama ‘nyundo’ kufanya hivyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic