March 2, 2013




Ingawa Kocha Mkuu wa Man United, Alex Ferguson alipinga kauli ya Roberto Mancini wa Man City kwamba timu yake ina bahati kuwa kileleni, lakini amekubali kuwa Real Madrid inamuweka roho juu.

Man United itacheza na Real Madrid katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya mechi ya  kwanza jijini Madrid kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kikosi cha United zaidi kinawategemea washambuliaji wawili, Robin van Persie anayeonekana yuko katika kiwango kizuri zaidi pamoja na Wayne Rooney ambaye pia anaonekana kuhofiwa zaidi na Madrid.

Ferguson raia wa Scotland amesema kasi ya Real Madrid hasa katika ushambuliaji wa kushitukiza au kaunta atak, ni hatari sana na wachezaji wake Cristiano Ronaldo, Mesut Ozil na Angel Di Maria ni hatari sana.

“Nilikwenda kushuhudia, Madrid ni hatari sana wakati wanaposhambulia kwa kushitukiza, wachezaji wake hao watatu ni hatari sana.

“Lakini ni suala la kulifanyia kazi na mambo yanaweza kufanya kazi. Hatupaswi kuogopa, badala yake tahadhari na mipango,” alisema Ferguson leo asubuhi.

Ferguson alikuwa kwenye Uwanja wa Camp Noun a kuihuhudia Barcelona ikiteseka dhidi ya Real Madrid na kulala kwa mabao 3-1.

Kila timu inaendelea na maandalizi ya mchezo huo ambao utakuwa moja ya mechi gumzo zinazosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka.

1 COMMENTS:

  1. angechezesha Web walaa wangekuwa na uhakika na ushindi ila duuu sie yeye

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic