March 2, 2013


Mabingwa wa Tanzania, Simba leo watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi yao ya kesho dhidi ya wenyeji wao Libolo.

Simba watafanya mazoezi kwenye Uwanja Manispaa ya Calulo ambako kesho ndiyo kutakuwa na kazi ngumu ya kuwang'oa Waangola, Libolo ambao walipata ushindi wa bao 1-0 katika mechi yao ya kwanza jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Simba, Evodius Mtawala amethibitisha vijana wake kuwa fiti, ingawa Mwinyi Kazimoto amepata maumivu makali ya jino na huenda akaukosa mchezo huo ingawa ni suala la kusubiri.

Lakini mmoja wa Simba mjini Calulo alisema kila kitu kinakwenda vizuri na Simba watafanya mazoezi kuanzia saa tisa alasiri ya Angola ambayo ni saa 10 kamili hapa nyumbani Tanzania.

Kwa mujibu wa mwenyeji huyo, tayari matangazo mitaani yametolewa kuwa mechi hiyo itachezwa saa 10 jioni hiyo kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic