March 2, 2013




Matajiri wa jiji la Paris, klabu ya PSG wameamua kufanya kufuru ili wamnase kiungo nyota wa Man City, Samir Nasri.
PSG waliingia vitani kumuwania Nasri mwaka 2011, lakini wakakwama baada ya kupigwa bao na Man City ambao walilipa mamilioni ya pauni kwa Arsenal na kumchukua.

Taarifa kutoka ndani ya Man City zimeeleza, Mkurugenzi wa ufundi wa PSG, Leonardo anavutiwa zaidi na Nasri na yuko tayari kuishawishi klabu hiyo kutoa hadi pauni milioni 24 kumnasa.

Pamoja na hivyo, mshahara wa Nasri ambao ni pauni 170,000 kwa wiki, hauwezi kuwa tatizo kwa mamilionea hao wa Ufaransa wenye wachezaji ghali na maarufu kama David Beckham na Zlatan Ibrahimovic.

Siku za hivi karibuni, Nasri amekuwa katika uhusiano mbaya na kocha wake, Roberto Mancini raia wa Italia ambaye aliamua kumshambulia Mfaransa huyo katika vyombo vya habari kwamba haridhishwi na kiwango chake.

Kitu kimeonyesha kumchanganya Nasri na PSG wameona ndiyo wakati mwafaka wa kumng’oa, ingawa uamuzi wa mwisho utaendelea kubaki kwake Nasri mara baada ya msimu huu kwisha.

1 COMMENTS:

  1. mchezaji yeyote akiondoka ilhali mzee wenger hakupenda basi huaga hafanikiwi yupo wapi flamin, jembe Jose antonio reyes,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic