Hatma ya African
Lyon kuendelea kushika mkia au la kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara itajulikana
kesho wakati itakapokuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Lyon ambayo imekuwa
ikipoteza michezo mfululizo ina pointi 13 kutokana na mechi 19 inabidi iifunge
Ruvu Shooting kama inataka kuirejesha mkiani Toto African yenye pointi 14. Kama
kweli inazitaka pointi zote tatu itabidi ifanye kazi mbele ya Ruvu Shooting
inayotiwa makali na Kocha Charles Boniface Mkwasa.
Hiyo itakuwa mechi
ya 18 kwa Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya saba ikiwa na pointi 26
ikitanguliwa na vinara wa ligi hiyo Yanga, Azam, Simba, Coastal Union, Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar yenye pointi 28 ikinolewa na nahodha wa zamani wa Taifa
Stars, Mecky Maxime.
Mechi hiyo namba
139 itachezeshwa na mwamuzi Amon Paul kutoka Musoma wakati wasaidizi ni Anold
Bugado wa Singida na Milambo Tshikungu kutoka Mbeya. Mwamuzi wa mezani atakuwa
Shafii Mohamed wa Dar es Salaam.
Nayo Tanzania
Prisons ya Jumanne Chale itakuwa mgeni wa Oljoro JKT katika mechi itakayochezwa
Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha wakati Mgambo Shooting
itaoneshana kazi na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Keshokutwa (Machi 7
mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa
mechi kati ya JKT Ruvu ya Kocha Charles Kilinda na Kagera Sugar.
Ligi hiyo
itaendelea tena Jumamosi ya Machi 9 mwaka huu kwa mechi mbili; Yanga vs Toto
Africans (Uwanja wa Taifa), na Azam vs Polisi Morogoro (Azam Complex, Chamazi).
0 COMMENTS:
Post a Comment