March 5, 2013



 Unaweza kusema utakapofikia wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Man United na wageni wao Real Madrid itakapoanza dunia ‘itasimama’, bei za tiketi zinaonekana kuwa tatizo.

Watu kadhaa ambao walinunua tiketi za mechi hizo mapema, wamefikia kuuza hadi pauni 1,000 (zaidi ya Sh milioni 2.4).
Watu kadhaa walionekana karimu na Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester wakiwa wamebandika mabango kuwa wanataka tiketi.


Baadhi ya mitandao pia ilikuwa ikitangaa kuhusiana na tiketi hizo zinazolanguliwa na watu waliendelea kuzinunua kutaka kuona kazi ya leo usiku kati ya Alex Ferguson dhidi ya Jose Mourinho.
Mtandao wa ticket4football.com ulieleza wazi kuhusiana na mauzo ya tiketi na watu wakaonekana kugombea.
 Asilimia kubwa ya mashabiki jijini Manchester wanataka kuona Ronaldo anataka kufanya vipi kazi yake leo usiku na kama ataweza kuikomboa Madrid ambayo katika mechi ya kwanza ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya bao 1-1.

Tiketi ambazo ziliuzwa halali kuanzia pauni 250, baadaye zilipanda haraka hadi kufikia pauni 750. Lakini hali inazidi kuonekana mbaya, kwani kadiri muda unavyosonga mbele huenda zikavuka zaidi ya pauni 1000.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic