March 2, 2013




Uongozi wa Libolo ya Angola wameonyesha wako tayari kumsajili kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa hata kabla ya mechi yao ya kesho dhidi ya Simba.

Libolo wameonyesha wana mchechezo baada ya kusisitiza wanamtaka Ngassa mara baada ya kutua katika jiji la Luanda lakini wakafanya hivyo baada ya Simba kuwasili katika mji wa Calulo ambako ni makao makuu ya timu hiyo. 

Katika mazungumzo yake na Poppe, Correia alisema wanataka kuzungumza na uongozi wa Simba lakini mwenyekiti wa usajili wa Simba, Zacharia Hans Pope amesisitiza mara zote, hilo litafanyika baada ya mchezo.

Ngassa alianza kuwavutia Waangola hao katika mechi ya kwanza wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa Dar na Simba ikalala kwa bao 1-0.

Simba iko tayari ya mchezo wa marudiano mjini humo, jana jioni ilifanya mazoezi kwenye uwanja tofauti lakini kesho lazima ifanye katika uwanja wa Estadio Municipal De Calulo ambao utachezewa mechi hiyo kesho Jumapili.

Ikiwa Angola, Simba itamkosa kiungo wake Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye aligua malaria na kuachwa jijini Dar wakati meneja wake, Moses Basena yeye amerejea kwao Kampala, Uganda kwa kuwa mkewe ni mgonjwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic