March 4, 2013



Okwi mazoezini juzi...

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ameendelea kufanya vizuri mazoezi na timu yake mpya ya Etoile du Sahel.

Ingawa hajaanza kuaminiwa kama ilivyokuwa wakati akicheza Simba, Okwi amekuwa akiendelea na mazoezi na wenzake kama kawaida.
Unapofikia wakati wa mechi, Mganda huyo huwasubiri wenzake wapambane lakini benchi la timu hiyo ya Tunisia wanajua wanachokifanya.

Alipotua nchini humo, mara baada ya kuanza mazoezi alipangiwa mazoezi ya kuongeza nguvu ikiwa ni pamoja na kasi ili kuweza kukabiliana na upinzani mkali we ligi ya nchi hiyo.

Okwi wakati anaondoka nchini alikuwa tegemeo la ushambuliaji la Simba, tokea ameondoka, inaonekana Wekundu wa Msimbazi wamekuwa wakiyumba kumpata mtu kama yeye ambaye atakuwa akianzisha mashambulizi ya nguvu.
Okwi aliuzwa kwa dola 300,000 kwa Etoile du Sahel, naye akalipwa dola 100,000 na amekuwa akila mshahara we dola 15,000 kwa mwezi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic