March 5, 2013




Naibu Waziri we Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla amesema Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ana matatizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Makalla alisema ana wasiwasi na maamuzi anayochukua Osiah kama yanaweza kuchukuliwa na mtu aliyetulia.

“Sidhani kama Angetile ni mzima vizuri, hivi karibuni nilikaa naye katika vikao kadhaa, kuna wakati nililazimika kumuokoa kutokana na maamuzi aliyokuwa anachukua.

“Mfano sasa anasema hana imani na mimi, lakini tulipozungumza na Tenga akasema tofauti. Ninaamini uamuzi wa Tenga ndiyo sahihi,” alisema Makalla.


“Hata kama watakuja wizarani kuzungumza, watanikuta mimi kwa kuwa waziri hatakuwepo nchini kwa siku kumi. Mimi ndiyo watanikuta.”

Jana TFF ilieleza kutokuwa na imani na Makalla kuhusiana na suala katiba yao mpya kukataliwa na serikali kutaka waitumie ile ya mwaka 2006.

Hivyo TFF, ikaomba itakapokwenda wizarani kuzungumza na serikali, Makalla asiyehusishwe na badala yake wazungumza waziri mwenyewe Dk Fenella Mukangara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic