March 9, 2013


Amepania kuonyesha anajua, Mario Balotelli jana ameingia na kuisaidia timu yake yua AC Milan kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Genoa.

Mechi hiyo ya Serie A iliyokuwa inaonekana ngumu, iliisha kwa AC Milan kuibuka na ushindi huo Balotelli akiwa amechangia bao moja.

Hata hivyo, Balotelli alionyesha ni mtukutu baada ya kulambwa kadi, dakika 30 tu baada ya kuingia uwanjani. Lakini akaonyesha pia anaiweza kazi yake kwa kufunga bao muhimu.

Hilo limekuwa bao la tano kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Man City, ambaye ameendelea kuonyesha ana uwezo mkubwa, tatizo kubwa limekuwa utukutu wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic