March 8, 2013



 Mudde wa tatu kushoto waliosimama..
Kiungo Mussa Mudde ameungana na wenzake katika kambi ya timu hiyo iliyo katika hoteli ya Sapphire, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mudde alipata msiba wa kufiwa na binti yake, hali iliyomlazimu kusafiri kwenda kwao Uganda kulishughulikia tatizo hilo.

Pamoja na Mudde, Meneja wa Simba, Moses Basena, naye ameungana na kikosi hicho baada ya kurejea kutoka kwao Kampala ambako alikuwa anauguliwa na mkewe.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amethibitisha hilo dakika chache zilizopita na kusema tayari wako kambini.

“Tuko kambini tokea jana, maandalizi yanaendelea na Mudde na Basena wameshaungana na wenzao kwa ajili ya kambi,” alisema Kamwaga.

Simba inatarajia kuivaa Coastal keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mechi ya kwanza, timu hizo zilitoka sare tasa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga huku wenyeji Coastal wakiutawala mchezo kwa kiwango kikubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic