March 3, 2013



Huku ikionekana kama itaamka, Arsenal ilijikuta ikilala kwa mabao 2-1 katika mechi ya Premiership, leo.
Mechi hiyo kubwa zaidi kwa Arsenal kwa maana ya utani wa jadi na Tottenham Hotspur ilikuwa nzuri na ya kuvutia kutokana na timu zote kucheza mchezo wa kasi.

Lakini Bale na Lennon ndiyo waliipatia mabao Spurs na mkongwe wa Kijerumani, Per Mertesacker akaifungia bao pekee. Kwa ushindi huo Spurs imesogea hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54, nyuma ya Man City katika nafasi ya pili na 56, huku vinara Man United wakiwa na 71.

Arsenal, maarufu kama vijana wa Wenger wanabaki katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 47, wakijaribu kupambana kuwavuka Chelsea wenye 51.
Kituko kingine kilichotokea katika mechi ya leo ni shabiki wa Arsenal kumrushia Bale ganda la ndizi ikiwa ni dalili ya ubaguzi wa rangi au kumfananisha mchezaji huyo na nyani au sokwe.

Kidogo, imeonekana si kitu cha kawaida kwa kuwa mashabiki wazungu hufanya hivyo kwa wachezaji weusi au wale wenye asili ya Afrika.

KESHO JUMATATU:
Aston Villa Vs Man City

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic