March 3, 2013

SEC HALF:
Dk 87 GOOOO, Vado tena.....Libolo wanapata bao la nne...safu ya ulinzi ya Simba ilishindwa kuwa shap kuondosha hatari langoni. Matumaini yamepotea na Simba wanaonekana kukata tamaa pia wanaonekana kuchanganyikiwa


Dk 82 GOOOO...Simba wanafungwa bao tatu, Ruben anapiga shuti kali nje ya 18 na kuandika bao ....
Dk 79 GOOOOO....Libolo wanapata bao la 2, Rasca aliyeingia kuchukua nafasi Joao Marting anafunga kiufundi kabisa...huku ikionekana hakuna matumaini kwa Simba kusonga mbele
Kipindi cha pili, Liewig ameamua kumtoa Kinje na kumuingiza Mwinyi Kazimoto ambaye alibaki nje kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya jino.
Libolo bado wanaongoza kwa bao hilo moja huku wakicheza mpira wa taratibu na mashambulizi ya kushitukiza.
Mechi imeanza kwa kasi ingawa maji yanaendelea kwua tatizo kubwa uwanjani.


FIRST HALF...Libolo 1-Simba 0
GOOOOOO.....Simba imefungwa bao moja katika dakika ya 8, mfungaji ni Vado baada ya kuunganisha krosi ya Ruben
Libolo wanaongoza...
Mechi kati ya Simba dhidi ya wenyeji wake Libolo imeanza, ila tatizo kulikuwa na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia asubuhi.

Mfaransa Patrick Liewig ameamua kuanza na wachezaji wafuatao, huku akitimiza ahadi yake ya kumuweka benchi nahodha Juma Kaseja na nafasi yake imechukuliwa na Abel Dhaira.

Kama haitoshi Mfaransa huyo ameshangaza zaidi kwa kuamua kuanza na mkongwe Salim Kinje ambaye amekuta hata hapati nafasi ya kucheza katika mechi za ligi.
WALIO UWANJANI SASA KATIKA MECHI HIYO NI ;
Abel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Komambil Keita, Juma Nyosso, Shomari Kapombe, Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Haroun Chanongo, Felix Mumba Sunzu na Salim Kinje.

SUB:
 Juma Kaseja, Kiggi Makasi, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Abdallah Juma. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic