March 25, 2013



Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia  kati ya Tanzania (Taifa Stars) na
Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jana (Machi 24 mwaka huu) na
Stars kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 226,546,000.


 Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 32,614 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha Sh 5,000, sh. 7,000, sh.
10,000, sh. 15,000, Sh 20,000 na Sh 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 34,557,864.41, maandalizi ya mchezo
sh. 28,450,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh.
8,625,641.88.


Nyingine ni bonasi kwa timu ya Taifa Stars sh. 28,798,220.34, asilimia
15 ya uwanja sh. 18,917,141.01, asilimia 20 ya gharama za mechi Sh
25,222,854.67 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) Sh 6,305,713.67.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Sh
71,885,135.82 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh 3,783,428.20 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic