Kocha
Mkuu wa Kenya, Adel Amrouche amewaonya Azam FC kuhusiana na uchezaji wa FAR
Rabat.
Azam
FC inawakaribisha FAR Rabat ya Morocco katika mechi ya Kombe la Caf, Jumamosi
kwenye Uwanja we Taifa, Dar.
Amrouche
ambaye ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika Kaskazini kwa kuwa asili yake ni
Algeria, amesema Wamorocco hasa upande wa klabu ni wepesi sana kwa kushambulia
haraka.
“Wanachotakiwa
Azam FC ni kucheza mpira wa kasi, kama watashindwa na kuiga wanachotaka wao
basi watapotea.
“Kingine
kwa kuwa Azam wanaanzia nyumbani, basi ni lazima wacheze na kuhakikisha
wanashinda mabao angalau matatu ili kujiweka katika nafasi nzuri,” alisema
Amrouche ambaye pia ana uzoefu na soka la ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
kwa kuwa amewahi kufanya kazi DR Congo, Burundi na sasa Kenya.
kwa
mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), FAR Rabat wanatarajiwa kuwasili
nchini kesho.
AS FAR KUWASILI KESHO KUIKABILI AZAM
Wapinzani wa Azam katika michuano ya Kombe la
Shirikisho, AS FAR Rabat ya Morocco wanatarajiwa kutua nchini kesho (Aprili 17
mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates.
Msafara wa timu hiyo wenye watu 28 utafikia hoteli ya
Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo ya
kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10
kamili jioni Uwanja wa Taifa.








0 COMMENTS:
Post a Comment