Ujumbe
wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) tayari uko nchini na umeanza kazi
yake.
Ujumbe
huo chini ya Mkuu wa Idara ya Uanachama wa Fifa, Primo Corvaro umewasili jana
nchini tayari kutatua mgogoro wa Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Msemaji
wa TFF, Boniface Wambura amesema Primo ameongozana na Mkuu wa Kanda hii,
Ashford Mamelodi.
“Wakiwa hapa watawendelea na
shughuli yao lakini wakiweza watakutana na Waziri mwenye dhamana ya michezo.
“Walijaribu kukutana naye
leo lakini ikashindikana kwa kuwa waziri yuko bungeni amebanwa na majukumu
mengine.
“Watajitahidi kukutana naye
lakini kama itashindikana basi, haina maana ni lazima wafanye hivyo lakini
wanakwenda kwa nia ya kwenda kumsalimia tu,” alisema Wambura.
Hata
hivyo, Wambura amesema Ujumbe huo wa FIFA umeshindwa kukutana na Waziri wa
Habari, Utamaduni na Michezo, D. Fenella Mukangara kwa kuwa hivi sasa yupo
Bungeni, Dodoma.
Kazi kubwa ya Corvaro na Mamelodi watakutana na wagombea
ambao wana malalamiko yao.
Wagombea
watakaosikilizwa ni Jamal Malinzi nayegombea Urais aliyepitishwa na Kamati ya Uchaguzi. Lakini akakatiwa
rufani iliyopitishwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, akaondolewa kwenye
mchakato wa uchaguzi.
Wengine
watakaosikilizwa ni Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura
ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na rufani yake kukataliwa na
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF.
Mgombea
wa nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ligi, Hamad Yahya aliyepitishwa na Kamati ya
Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na kuondolewa. Aliomba shauri lake liangaliwe
upya, lakini Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF ikatupa ombi lake.
Mgombea
wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji, Farid Salim Mbaraka ambaye alienguliwa na Kamati ya Uchaguzi na
baadaye rufani yake kwa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kutupwa na hali
kadhalika ombi lake la kutaka shauri lake liangaliwe upya, kukataliwa.
RATIBA YA UJUMBE WA FIFA NCHINI
Tarehe /Muda
|
Tukio
|
15 Aprili 2013
Saa 12:30 – 03:00
|
Kuwasili kwa wajumbe wa FIFA
|
15 Aprili 2013
Saa 04:00 – saa 05:00 usiku
|
Kikao na Rais wa TFF pamoja na Sekretarieti
|
16 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30 asubuhi
|
Kukutana na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupata taarifa ya uchaguzi
|
16 Aprili 2013
Saa 06:30 – 08:00 mchana
|
Chakula cha Mchana
|
16 Aprili 2013
Saa 08:00 – 12:00 jioni
|
Kukutana na wagombea walioondolewa
|
17Aprili 2013
Saa 03:00 – 05:00 asubuhi
|
Kukutana na Kamati ya Rufaa za Uchaguzi ya TFF
|
17 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30
Mchana
|
Kupewa taarifa zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi, i.e., kesi zilizo mahakamani
|
17 Aprili 2013
Saa 08:00 – 10:00 jioni
|
Kukutana na watu wengine ambao FIFA wanaweza kuomba kukutana nao
|
17Aprili 2013
Saa 10:30 – 11:00 jioni
|
Mkutano na waandishi wa habari – kushukuru mamlaka na pande zilizohusika kwa ushirikiano
|
18 Aprili 2013
Saa 10:00 – 12:00 Alfajiri
|
Kuondoka hotelini kwa ajili ya safari
|







0 COMMENTS:
Post a Comment