Hii ndiyo ilikuwa picha ya kuvutia zaidi katika mechi kati ya Simba dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa Jumapili iliyopita.
Inaonekana Humprey
Mieno ‘Hum’ raia wa Kenya akijaribu kumpokonya mpira kinda wa Simba, Abdallah
Seseme bila ya mafanikio, lakini kabari aliyompiga ndiyo kivutio zaidi.
Kiasi fulani
mwamuzi, Oden Mbaga aliuchuna lakini akaona Mieno anaweza kuua, hivyo
akalazimika kupiga filimbi.
Mechi hiyo
ya kuvutia ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2, Simba ikitangulia kufunga yote
mawili katika kipindi cha kwanza na Azam FC ikasawazisha katika kipindi cha
pili.
PICHA NA
CHAMPIONI NEWSPAPER







0 COMMENTS:
Post a Comment