| Abdul (kulia) akiwa na Luhende naTelela.. |
Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amelazimika kuendelea kubaki nje
katika kikosi cha Yanga kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.
Abdul aliyejiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, anaendelea
na matibabu.
Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Nassor Matuzya, beki huyo huenda akaanza
mazoezi mepesi kesho.
“Matibabu yanakwenda vizuri na kama kila kitu kitaenda kama
tulivyopanga, basi huenda kesho asubuhi akaanza mazoezi,” alisema Matuzya.
Pamoja na Abdul, mshambuliaji Didier Kavumbagu jana alianza mazoezi
maalum wakati kikosi cha Yanga kinajifua kwenye Uwanja wa Loyola, Mabibo,
Dar.
Wakati wenzake walikuwa wakifanya mazoezi pamoja, Kavumbagu alikuwa
akikimbia taratibu na Matuzya alisema hiyo ni programu maalum.
Kavumbagu alikuwa anasumbuliwa na maumivu makali ya msuli kamba ambao
ulimuweka nje kwa siku kadhaa.







0 COMMENTS:
Post a Comment