April 20, 2013




Hali ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima bado haijatengemaa vizuri.
Kiungo huyo leo alilazimika kufanya mazoezi baada ya Kocha Ernie Brandts kufanya mazungumzo kwa muda na daktari wa timu, Nassor Matuzya.


Baada ya mjadala huo, Brandts aliruhusu afanye mazoezi lakini Dk Matuzya alilazimika kumuwekea plasta kwenye pua yake ambayo ilionyesha ina jeraha.

Katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mugambo Shooting, Niyonzima alikaa benchi ingawa baada ya hali kuwa ngumu akaingia na kusaidia kupatikana kwa bao la kusawazisha.


Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga ilimalizika kwa sare ya mabao 1-1 na kupunguza kasi ya Yanga ambayo inakwenda kasi kutwaa ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic