DK 89,90,
Azam FC wanaendelea kupoteza nafasi za wazi, mwisho mechi inamalizika kwa sare
ya bila kufungana. Maana yake Azam FC inasonga mbele kutokana na ushindi wake
wa ugenini wa mabao 3-1.
Dk 83, Tchetche naye anapoteza nafasi ya wazi.
Dk 67,
Bolou anakosa bao la wazi, alimpa pasi Mieno, naye akamrudishia, walinzi wa BYC
wakadhani ameotoa, hivyo akasogea kabisa karibu na kipa, akiwa ndani ya 18
akitazamana na kipa, akaupaisha mpira..buuuuuu..
Dk 51,
Faulo maridadi iliyopigwa na Mcha, mpira unamfikia Bocco, akiwa katika nafasi
nzuri anajigonga miguu hadi mpira unatoka.
Dk 46, Azam
wanamtoa Umonyi, nafasi yake inachukuliwa na Mcha.
MAPUMZIKO 0-0:
Dk 41,
Mieno anachonga kona safi, inayotua kwa Atudo, anapiga kisigino saaafi, lakini
mpira unagonga mwamba na kuokolea.
Dk 33,
Bocco anawatoka mabeki wa BYC, anatoa pasi nzuri kwa Mieno ambaye anaudokoa
mpira unaompita kipa, lakini wakati ukielekea kuvuta mstari, anatokea beki na
kuukoa.
Dk 26, BYC
wanafanya shambulizi kali na mpira wa shuti la Barshal linapanguliwa na Mwadini
na kuwa kona ambayo haikuwa na majibu.
Dk 11,
Tchetche anawatoka mabeki wawili na kupiga krosi lakini mpira wa kichwa wa Umonyi
unadakwa na kipa vizuri.
Mechi
inaanza kwa mashambulizi ya zamu lakini kila timu haijatulia.
0 COMMENTS:
Post a Comment