Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts leo ameanza
mazoezi na kikosi chake.
Brandts amerejea mazoezini baada ya kulazimika
kulala nyumbani kwa siku nne kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Leo asubuhi alikuwa katika mazoezi ya Yanga kwenye
Uwanja wa Loyola jijini Dar akiendelea na kazi yake.
Jana usiku, Brandts alisema amerejea katika hali
nzuri ingawa bado hakuwa na nguvu ya kutosha.
“Natarajia kuanza kazi kesho asubuhi, kidogo naona
niko vizuri. Tatizo ni ngumu lakini mambo mengine yatarekebika wakati naendelea
na kazi,” alisema.
Lakini leo mchana Brandts alisema: “Nimeanza
kujisikia vizuri kwa kiasi kikubwa, lakini naona bado sijawa vizuri.
“Nahitaji kunywa maji mengi lakini sina ujanja
lazima niwe kazini kwa kuwa tunakwenda mwisho wa msimu.
“Nimekuwa na maumivu makali kwa kuwa hii ni mara
yangu ya kwanza kuugua ugonjwa wa malaria, kila kitu nilikiona kigeni.”
Katika mechi kati ya Yanga na Ruvu JKT, Kocha
Msaidizi alipewa jukumu la kuongoza kikosi baada ya Brandts kuzidiwa. Katika
mechi hiyo Yanga ilishinda kwa mabao 3-0.







0 COMMENTS:
Post a Comment