![]() |
| Akiwa na Fidel Castro... |
Diego
Maradona juzi aliamua kumtembelea Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro nyumbani
kwake mjini Havana.
Maradona
ambaye alifunga mabao 34 katika mechi 91 alizoichezea timu ya taifa ya Argentina,
alimtembelea rais huyo maarufu duniani kote na kufanya naye mazungumzo.
Maradona amekuwa rafiki mkubwa na mtu anayeunga mkono siasa za mfumo wa Castro ambaye ni mmoja wa wakomunisti ngangari.
Pamoja na kumtembelea Castro, Maradona alitua nchini Venezuala na kumuunga mkono mgombea wa urais aliyekuwa anaunga mkono siasa za marehemu Hugo Chavez ambaye alishinda uchaguzi huo.
![]() |
| Akiangana na Rais Maduro wa Venezuala.. |
Maradona
alimtembelea na kushiriki katika kampeni za Nivolas Maduro, kabla ya uchaguzi
huo ambao baadaye aliibuka mshindi.
Akiwa
na Maduro, Maradona alimkabidhi jezi ya Argentina na kumuambia amfikishie
salama za pole na msamaha kwa familia ya Chavez kwa kuwa alishindwa kuhudhuria
mazishi.











0 COMMENTS:
Post a Comment