Milipuko
miwili imeua watu jana jioni kwenye mashindano ya riadha ya Boston Marathoni
nchini Marekani.
Milipuko
hiyo hatua kadhaa kutoka katika sehemu ambayo wanariadha walitakiwa kumaliza.
Katika
mlipuko huo ambao umeleta hali ya taharuki nchini Marekani, watu saba
wameripotiwa kupoteza maisha hadi leo asubuhi.
Wengine
144 walitangaza kujeruhiwa na kati yao, 17 walikuwa wamejeruhiwa vibaya sana.
Hata
hivyo, mshindi alikuwa amemaliza zaidi ya saa moja na baadhi ya wanariadha
wakiendelea kuwasili, mlipuko wa kwanza ulitokea.
Baadaye
mlipuko mwingine ulifuatiwa wakati majeruhi wa mlipuko wa kwanza wakiendelea
kuokolewa.
TUNAOMBA
RADHI KWA PICHA AMBAZO ZINATISHA, LAKINI NDIYO HALI HALISI YA TUKIO
HILO.















0 COMMENTS:
Post a Comment