Mabingwa
watetezi wa Tanzania Bara, Simba, leo wameendelea na mazoezi kujiwinda na mechi
zilizobakia za mzunguko wa pili.
Chini ya
Kocha Mkuu, Patrick Liewig raia wa Ufaransa na Msaidizidi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’,
Simba ilifanya mazoezi katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Inaonekana Simba
imepoteza matumaini ya kutetea ubingwa wake huo huku Yanga na Azam FC ndiyo
zikifukuzana kileleni.
Tayari
Simba iko katika nafasi ya nne lakini imeapa kupambana angalau kupata nafasi ya
pili ili ishiriki michuano ya kimataifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment