Baada ya kutojitambua kwa zaidi ya saa 24, hatimaye Dzhokhar
Tsarnaev ameamka na kuanza kuhojiwa na maofisa wa usalama wa Marekani.
Maofisa hao wamekuwa wakimhoji Dzhokhar ,19, ambaye
ni mtuhumiwa wa pili wa ulipuaji wa bomu la Boston Marathoni.
Kaka yake aliuwawa wakati akipambana na polisi, lakini
Dzhokhar ameamka na kuanza kuhojiwa kwa
kutumia maandiko.
Maofisa wa polisi wamesema wamekuwa wakimhoji kwa
kuandika naye anajibu.
Hata hivyo inaonekana bado hawajajua mambo mengi
lakini amewaeleza kwamba hakutaka kukamatwa akiwa hai.
Ndiyo maana aliweka bunduki katika mdomo wake na
kujilipua akiwa na nia ya kujiua lakini hali haikwenda kama alivyotaka.
Wakati anakamatwa Dzhokhar alikuwa amepoteza damu nyingi na sasa yuko
katika hospitali moja mjini Boston ambako kuna ulinzi mkali sana.
Kaka yake Tamerlan ,26, aliuwawa wakati akipambana na polisi baada ya wawili hao kugundulika walihusika na ulipuaji wa mabomu mawili siku ya mashindano ya Boston Marathon jijini Boston,











0 COMMENTS:
Post a Comment