Kitendo cha mshambuliaji wa Liverpool kumuuma beki Branislav Ivanovic wa
Chelsea kimeanza kuzua madhara kwa watoto barani Ulaya.
Mtoto mmoja amemuuma mwenzake walipokuwa wakipigana shuleni na mama wa
mtoto aliyeng’atwa ametupa lawama moja kwa moja kwa Suarez.
Mama huyo amesema amepigiwa simu kutoka shuleni kwamba mwanaye ameng’atwa
na mwenzake.
“Lakini mwalimu kaniambia tukio lilikuwa kama lile la Suarez na beki wa
Chelsea,” alisema mama huyo alipozungumza na BBC 5Live.
Tayari watoto kadhaa wamekuwa wakionywa kutoiga tukio hilo la Suarez
kwani linaweza kuwaletea madhara.
Tayari Suarez amepigwa faini na
Liverpool kutokana na kitendo hicho lakini hata FA imetangaza kumuadhibu na
watu kadhaa wamekuwa wakilaani kitendo hicho kufanywa na mtu mzima kama yeye,
tena baba wa mtoto mmoja.








0 COMMENTS:
Post a Comment