Shirikisho
la Soka Ulaya (Uefa) liko katika hatua ya mwisho kupitisha sheria mpya ambayo
itakuwa ni kali kwa wabaguzi wa rangi katika mchezo wa soka.
Katibu Mkuu
wa Uefa, Gianni Infantino amesema kupitia sheria hiyo mpya, wachezaji,
mashabiki na hata viwanja vitakumbana na adhabu kali.
Alisema kiasi
cha chini kabisa katika adhabu hiyo mpya kwa mchezaji itakuwa ni kufungiwa
mechi kumi.
Wiki iliyopita, Rais wa Fifa, Sepp Blatter alisisitiza kuwepo kwa adhabu kali kwa wale wanaoendelea masuala ya ubaguzi wa rangi katika soka.
Msimu uliopita, John Terry wa Chelsea alifungiwa mechi nne kutokana na vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya Antoni Ferdinand na Mruguay, Luis Suarez we Liverpool akafungiwa kucheza mechi nane kwa kumfanyia vitendo vya kibaguzi, Patrice Evra wa Manchester United.
Vitendo vya
ubaguzi wa rangi vimekuwa vikichukua nafasi kila kukicha, wakati fulani Muitaliano
Mario Balotelli alitishia kumuua mtu yoyote atakayemfanyia vitendo vya ubaguzi wa
rangi, hata hivyo kauli hiyo haikusaidia kwani walimtupia ganda la ndizi.
0 COMMENTS:
Post a Comment