Kuna kila dalili mshambuliaji Mrusi wa Arsenal, Andrey Arshavin hana hamu ya kubaki Arsenal.
Mkataba wake umebaki miezi miwili na Arsenal imekubali aondoke kwa kuwa ni kati ya wachezaji wamekuwa wakilipwa mamilioni ya fedha bila ya yeye kufanya kazi.
Arshavin amekuwa akilipwa kitita cha pauni 95,000 kwa wiki ambayo ni fedha inayotokana na malipo ya tiketi za mechi za Arsenal ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na mashabiki kwamba ni ghali sana.
Kwa kuwa katika msimu huu amecheza dakika 341 pekee, maana yake Arshavin kwa kila dakika aliyoichezea Arsenal alikuwa analipwa pauni 7,800(zaidi ya Sh milioni 20.2).
Na kama ikigawanywa kwa saa aliitumikia Arsenal kwa kiasi gani, maana yake alikuwa akilipwa pauni 60,000 kila saa moja au dakika 60.
Kwa mwaka 2013, Arshavin mwenye miaka 31 ameichezea Arsena mechi moja kwa dakika 15 na ilikuwa Januari dhidi ya Chelsea na timu yake ikapokea kipigo cha mabao 2-1.
Kumekuwa na taarifa Mrusi huyo atastaafu lakini inaonekana huenda akarejea kwao Urusi na kuendelea kucheza soka katika timu mbalimbali za nchini mwake.
0 COMMENTS:
Post a Comment