April 10, 2013



 
Borussia Dortmund ya Ujerumani ndiyo timu inayoaminika kuwa na mashabiki wengi zaidi wanaoyoiunga mkono na wamekuwa nayo bega kwa beka katika kila mechi.
Mafanikio yao ya kufuzu hadi nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tena katika dakika mbili za mwisho imekuwa ni faraja kubwa kwa mashabiki wao.

Borussia maarufu kama ukuta wa njano, wanatumia rangi za njano na nyeusi na kila mechi inayowahusu, uwanja huonekana kuna rangi aina mbili tu. Hiyo inatokana na mashabiki kujitokeza kwa wingi zaidi.


Katika mechi yao ya jana dhidi ya Malaga, mashabiki hao waliingia uwanjani wakiwa na bango maalum lenye picha ya mtu akiwa na darubini.

Bango hilo limeelezwa kuwa bora na lenye mvuto zaidi kuliko yote ambayo yamewahi kuonekana uwanjani.
 
Bango la Urusi...
Baadhi yamekuwa yakiashiria ubabe, kama lile ambalo hutumiwa na mashabiki wa timu ya taifa ya Urusi au lile wanalotumia mashabiki wa timu ya taifa ya Serbia.
Lile la Borussia, linaonyesha amani tu lakini aliyeshika darubini anaonyesha ishara ya kuwa wao wanamuona kila mtu na wamejiandaa na tayari pongezi zimemiminika kwa waliolibuni.
 
Bango la Serbia...

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic