Man United bingwa, imewapoka jirani zake wenye makelele ubingwa wa Ligi
Kuu England, maarufu kama Premiership.
Inawezekana yakawa ni maumivu ya moyo kwa mashabiki wa Arsenal kwa
kumuona mshambuliaji wao wa zamani Robin van Persie akifunga mabao matatu
katika kipindi cha kwanza na kuihakikishia Man United kuwa bingwa wa England.
Lakini inaweza kuwa furaha kwa van Persie aliyesema anayataka makombe, akaamua
kuondoka Arsenal na sasa alichokisema kimetimia.
Katika mechi dhidi ya Aston Villa iliyomalizika muda mchache uliopita,
van Persie ndiye amekuwa chachu baada ya kufunga mabao hayo matatu muhimu.
Hadi Man United inakwenda mapumziko ilikuwa inaongoza kwa mabao hayo
matatu ya Mholanzi huyo yaliyofungwa katika dakika za 2, 13 na 33.
Kutokana na uchezaji wa United, dalili zote zilionyesha Aston Villa hawakuwa
na uwezo wa kuwazuia tena Mashetani hao wekundu.
Kipindi cha pil, Aston Villa walionekana kujitutumua kutaka kusawazisha
lakini baadaye wakazidi kulegea na kuifanya Man United izidi kuwapa kazi ya
kuokoa kila baada ya dakika chache.
Kwa ushindi huo Man United ilifikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa
na timu yoyote. Angalau City ikishinda mechi ilizobakiza inaweza kufikisha
pointi 83.
Tayari inaonekana nafasi mbili za juu zimeishajaa na waliokuwa mabingwa
watetezi Man City wanabaki kuwa na pointi 68 zinazowahakikishia kushika nafasi
ya pili.












0 COMMENTS:
Post a Comment