Pamoja na
kukubaliana na matokeo ya mechi ya jana dhidi ya Azam, uongozi wa Simba
unapenda kuweka rekodi wazi kwamba haukuridhishwa na uchezeshaji wa mwamuzi,
Oden Mbaga, hasahasa katika kipindi cha pili.
Kwa bahati
nzuri, msimamo huu wa Simba hauna hata chembe ya ushabiki kwa vile hata
washabiki waliokuwa katika upande wa watani wetu wa jadi, nao pia walionekana
kutofurahishwa na uchezeshaji wa Mbaga.
Mbaga ni
mwamuzi mwenye beji ya Shirikisho la Kimataifa (Fifa) na katika hali ya kawaida
ilitazamiwa mechi ingechezeshwa kwa viwango vya kimataifa lakini hali ilikuwa
kinyume chake.
Simba
inaamini kwamba Mbaga hakuutendea haki mchezo ule wa jana. Simba inasema hivi
kwa sababu inataka mwamuzi huyo ajirekebishe na kwamba matokeo ya mechi
viwanjani yaamuliwe na ubora wa timu na si maamuzi yenye utata.
EZEKIEL KAMWAGA
MSEMAJI SIMBA








0 COMMENTS:
Post a Comment